وَأُمۡلِي لَهُمۡۚ إِنَّ كَيۡدِي مَتِينٌ
Nami nitawapa muda. Hakika mpango wangu ni madhubuti.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na nitawapa muhula hawa ambao walizikanusha aya zetu mpaka wadhanie kwamba wao hawatateswa, waongeze ukafiri na uasi. Na kwa hivyo, waongezewe adhabu. Kwani vitimbi vyangu ni vigumu, yaani: ni vya nguvu na vikali havizuiliwi kwa nguvu wala kwa hila.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس