Tafsiri ya Sura Al-Fil kwa السواحلية kutoka الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Verse 1
Je hujui, ewe Mtume, namna Alivyowafanya Mola wako watu wa ndovu: Abraha Mhebeshi na jeshi lake ambalo alikuja nalo ili kuivunja Alkaba tukufu?
Verse 2
ﮕﮖﮗﮘﮙ
ﮚ
Kwani Hakuijaalia mipango yao mibaya waliyoifanya ni yenye kuvunjika na kupita patupu?
Verse 3
ﮛﮜﮝﮞ
ﮟ
Na Aliwapelekea makundi yaliyofuatana,
Verse 4
ﮠﮡﮢﮣ
ﮤ
ya ndege waliokuwa wakiwatupia wao vijiwe vya udongo mkavu mgumu.
Verse 5
ﮥﮦﮧ
ﮨ
Akawapondaponda, wakawa ni kama majani makavu yaliyoliwa na wanyama na halafu kutupwa.
تقدم القراءة