Tafsiri ya Sura At-Tur kwa السواحلية kutoka الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Verse 1
ﮞ
ﮟ
Anaapa Mwenyezi Mungu kwa Ṭūr, nalo ni jabali ambalo juu yake Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, Alizungumza na Mūsā.
Verse 2
ﮠﮡ
ﮢ
Na kwa Kitabu kilichoandikwa, nacho ni Qur’ani,
Verse 3
ﮣﮤﮥ
ﮦ
kwenye nyaraka zilizokunjuliwa.
Verse 4
ﮧﮨ
ﮩ
Na kwa Nyumba Iliyoamirishwa kwa Malaika watukufu wenye kuizunguka daima.
Verse 5
ﮪﮫ
ﮬ
Na kwa sakafu iliyoinuliwa juu, nayo ni uwingu wa duniani.
Verse 6
ﮭﮮ
ﮯ
Na kwa bahari iliyowashwa moto, iliyojaa maji.
Verse 7
ﮰﮱﯓﯔ
ﯕ
Hakika adhabu ya Mola Wako, ewe Mtume, ni yenye kuwashukia makafiri.
Verse 8
ﯖﯗﯘﯙ
ﯚ
Hakuna kizuizi cha kuizuia itakaposhuka.
Verse 9
ﯛﯜﯝﯞ
ﯟ
Siku ya mbingu kutetemeka mpango wake kuharibika na pande zake kusukikasukika, na hapo ni wakati wa mwisho wa dunia,
Verse 10
ﯠﯡﯢ
ﯣ
na majabali yaondoke mahali pake na yatembee kama vile mawingu yanavyotembea.
Verse 11
ﯤﯥﯦ
ﯧ
Maangamivu katika Siku hii ni yenye kuwashukia wakanushaji.
Verse 12
ﯨﯩﯪﯫﯬ
ﯭ
Ambao wao wamevama ndani ya ubatilifu wanapumbaa nao na wanaifanya dini yao kuwa ni shere na mchezo.
Verse 13
ﯮﯯﯰﯱﯲﯳ
ﯴ
Siku ya kusukumwa hawa wakanushaji msukumo wa nguvu wenye kuwadhalilisha hadi kwenye Moto wa Jahanamu.
Verse 14
ﯵﯶﯷﯸﯹﯺ
ﯻ
Na waambiwe kwa njia ya kuwalaumu na kuwakaripia, «Huu ndio huo Moto ambao mlikuwa mkiukanusha!
Verse 15
ﭑﭒﭓﭔﭕﭖ
ﭗ
«Je, ni uchawi adhabu hii mnayoishuhudia au nyinyi hamtazami?
Verse 16
Onjeni ukali wa Moto huu. Vumilieni uchungu wake na ukali wake au msiyavumilie hayo, hamtahafifishiwa adhabu na hamtatoka humo. Ni sawasawa kwenu nyinyi mkivumilia au mkitovumilia. Hakika nyinyi mnalipwa tu yale mliokuwa mkiyafanya duniani.
Verse 17
ﭦﭧﭨﭩﭪ
ﭫ
Hakika wachamungu watakuwa kwenye mabustani ya Pepo na neema kubwa.
Verse 18
Watajistarehesha kwa vile Alivyowapa Mwenyezi Mungu vya neema miongoni mwa aina mbalimbali za ladha na starehe, na Atawaokoa mwenyezi Mungu kutokana na adhabu ya Moto.
Verse 19
ﭵﭶﭷﭸﭹﭺ
ﭻ
Kuleni chakula kwa furaha, na mnywe kinywaji chenye ladha, yakiwa ni malipo ya matendo mema mliyoyafanya duniani
Verse 20
Na wao watakuwa wametegemea, wako juu ya vitanda vinavyoelekeana, na tutawaoza wanawake weupe wenye macho mapana yaliyo mazuri.
Verse 21
Na wale walioamini na wakafuatwa na watoto wao katika hiyo Imani, Tutawakutanisha watoto wao nao katika daraja yao Peponi, hata kama hawakufikia matendo ya wazazi wao, ili wazazi wafurahike na watoto wao pamoja na wao katika daraja zao. Watakusanywa baina yao kwenye hali nzuri zaidi, na hatutawapunguzia chochote katika matendo yao mema. Kila mtu anafungwa na matendo yake aliyoyachuma, hatobeba dhambi za watu wengine..
Verse 22
ﮚﮛﮜﮝﮞ
ﮟ
Na tutawaongezea, juu ya starehe hizo zilizotajwa, matunda na nyama miongoni mwa vitu vinavyopendwa na kutamaniwa.
Verse 23
Na miongoni mwa starehe hizo ni kuwa wao watapeana gilasi ya pombe, mmoja wao atampa mwenzake, ili furaha yao ikamilike. Kinywaji hiki kinatafautiana na pombe ya duniani, hakimleweshi akili mwenye kukinywa, wala hakisababishi kubobokwa, wala maneno ya makosa na maasia.
Verse 24
Na watawazunguka watumishi waliotayarishwa kuwatumikia kama kwamba wao katika usafi na weupe na utungaji nidhamu ni lulu iliyohifadhiwa kwenye mashaza yake.
Verse 25
ﯓﯔﯕﯖﯗ
ﯘ
Watageukiana watu wa Peponi kuulizana wao kwa wao juu ya ukubwa wa yale waliyonayo na sababu ya kuyapata.
Verse 26
Watasema, «Sisi tulikuwa kabla, huko duniani, na sisi tuko baina ya watu wetu, tunamuogopa Mola wetu, tuna hadhari na adhabu Yake na mateso yake Siku ya Kiyama.
Verse 27
ﯡﯢﯣﯤﯥﯦ
ﯧ
Mwenyezi Mungu Akatuneemesha kwa uongofu na taufiki na Akatuokoa na adhabu ya vuke la Jahanamu, nalo ni moto wake na joto lake. Sisi tulikuwa, hapo kabla, tukimnyenyekea Yeye Peke Yake, hatumshirikishi na Yeye yoyote asiyekuwa Yeye, Atulinde na adhabu ya vuke la Motoni na Atupeleke kwenye starehe ya Peponi.
Verse 28
Mwenyezi Mungu Akatukubalia maombi yetu, na Akatupa tulichokiomba. Hakika Yeye Ndiye Mwingi wa kheri, Mwenye kurehemu. Na miongoni mwa wingi wa kheri Zake na rehema Zake kwetu ni kule kutupa radhi zake na Pepo, na kutuepusha na hasira Zake na Moto.»
Verse 29
Basi wawaidhie, ewe Mtume, wale uliotumilizwa kwao kwa Qur’ani, kwani hukuwa wewe, kwa neema ya Mwenyezi Mungu Aliokuneemesha kwayo ya unabii na busara ya akili, ni kuhani anayetoa habari za ghaibu bila ujuzi wala mwendawazimu asiyejua analolisema, kama wanavyodai.
Verse 30
Au wanakwambia hao washirikina, ewe Mtume, «Yeye ni mshairi, tunangojea ashukiwe na mauti»?
Verse 31
ﰄﰅﰆﰇﰈﰉ
ﰊ
Waambie, «Yangojeeni mauti yangu, kwani mimi pamoja na nyinyi ni katika wenye kuingojea adhabu yenu, na mtaona ni nani atakayekuwa na mwisho mwema.
Verse 32
Au zinawaamuru akili zao, hao wakanushaji, ziseme neno hili linalogongana (kuwa sifa ya ukuhani, utungaji mashairi, na wendawazimu haiwezekani kukutana wakati mmoja)? Bali wao ni watu waliruka mipaka katika uasi.
Verse 33
Au wanasema hawa washirikina, «Muhammad Ameibuni Qur’ani yeye mwenyewe?» bali wao hawaamini. Na lau wangaliamini, hawangalilisema walilolisema.
Verse 34
ﭣﭤﭥﭦﭧﭨ
ﭩ
Basi na walete maneno mfano wa Qur’ani iwapo wao ni wakweli katika madai yao kuwa Muhammad Ameibuni.
Verse 35
Je, wameumbwa hawa washirikina bila kuwako mwenye kuwaumba na kuwapatisha au wao wamejiumba wenyewe? Na yote mambo mawili haya yametanguka na hayawezekani. Na kwa hivyo, inalazimika kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Aliyewaumba, na Yeye Peke Yake Ndiye Ambaye hakuna anayepasa kuabudiwa, wala kufaa kuabudiwa, isispokuwa Yeye.
Verse 36
Au wao wameumba mbingu na ardhi kwa utengezaji huu wa kipekee? Bali wao hawaamini adhabu ya Mwenyezi Mungu, kwa kuwa wao ni washirikina.
Verse 37
Au wanazo wao hazina za Mola wako wanazitumia? Au wao ni majebari wanaowagandamiza viumbe vya Mwenyezi Mungu kwa kuwatendesha nguvu na kuwanyanyasa? Mambo si hivyo, bali wao ndio walemevu walio madhaifu.
Verse 38
Au wao wana ngazi ya kupandia mbinguni wanasikiliza huko wahyi kwamba yale waliyonayo ndio haki? Basi na aje, yule anayedai kuwa amesikia hilo, na hoja ya waziwazi yenye kusadikisha madai yake.
Verse 39
ﮏﮐﮑﮒﮓ
ﮔ
Je, mwenyezi Mungu , aliyetakasika, Ana watoto wa kike na nyinyi mna watoto wa kiume kama mnavyodai kwa uzushi na urongo?
Verse 40
Au je unawataka, ewe Mtume, hawa washirikina wakupatie malipo ya kuwafikishia Ujumbe, wakawa wao wana tabu na dhiki ya kujilazimisha malipo unayoyataka kutoka kwao?
Verse 41
ﮝﮞﮟﮠﮡ
ﮢ
Au je wao wana ujuzi wa ghaibu wakawa wanawaandikia watu na kuwapa habari yake? Mambo si hivyo, kwani hakika ya mambo ni kwamba hakuna anayejua ghaibu iliyo mbinguni na ardhini isipokuwa Mwenyezi Mungu.
Verse 42
Bali wao wanataka kumfanyia vitimbi Mtume wa Mwenyezi Mungu na Waumini. Basi hao makafiri, vitimbi vyao na njama zao vitawarudia wao wenyewe.
Verse 43
Au wao wana muabudiwa anayestahiki kuabudiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu? Ametakasika Mwenyezi Mungu na kutukuka na yale wanayoshirikisha. Kwani Yeye Hana mshirika katika mamlaka, na Hana mshirika katika Upweke na ustahiki wa kuabudiwa.
Verse 44
Na wakikiona hawa washirikina kipande cha mbingu kinawaangukia, kikiwa ni adhabu kwao, hawataacha yale waliyo nayo ya ukanushaji, na watasema, «Haya ni mawingu yamekusanyika na kupandana.»
Verse 45
Basi waache, ewe Mtume, hawa washirikina mpaka wakutane na Siku yao hiyo ya wao kuangamizwa, nayo ni Siku ya Kiyama.
Verse 46
Katika Siku hiyo havitawazuilia wao vitimbi vyao kotokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu kitu chochote, na hatawanusuru yoyote kuwaokoa na adhabu ya Mwenyezi Mungu.
Verse 47
Hakika madhalimu hawa watakuta adhabu duniani, kabla ya adhabu ya Siku ya Kiyama, ya kuuawa, kukamatwa mateka, adhabu ya kaburini na nyinginezo. Lakini wengi wa watu hawajui hilo.
Verse 48
Na uivumilie, ewe Mtume, hukumu ya Mola wako na amri Yake juu ujumbe Aliyokubebesha na juu ya makero yanayokupata kutoka kwa watu wako, hakika wewe uko kwenye maangalizi yetu, hifadhi na utunzi. Na umtakase Mola Wako kwa kumsifu unaposimama kuswali na unapoinuka kutoka usingizini.
Verse 49
ﰋﰌﰍﰎﰏ
ﰐ
Na kwenye kipindi cha usiku mtakase Mola wako kwa kumsifu, umtukuze na umswalie. Na ufanye hayo kwenye kipindi cha Swala ya Asubuhi wakati wa nyota kuondoka. Katika aya hizi pana kuthibitisha sifa ya macho mawili kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kwa inavyonasibiana na Yeye, bila kufananisha na viumbe Vyake au kuieleza dhati Yake vile ilivyo, kutakasika na kila sifa ya upungufu ni Kwake na sifa njema zote ni Zake, kama lilivyothibiti hilo katika Sunnah na kukubaliana juu yake wanavyuoni waliopita wa Ummah huu.
تقدم القراءة