سورة الكوثر

الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس

Tafsiri ya Sura Al-Kausar kwa السواحلية kutoka الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس

الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس

Verse 1
Sisi tumekupa, ewe Nabii, kheri nyingi za dunia na Akhera, miongoni mwazo ni mto wa Kauthar ulioko Peponi ambao pambizo zake ni mahema ya lulu na mchanga wake ni miski.
Verse 2
Basi, mtakasie Mola wako ibada yako yote na uchinje mnyama wako kwa ajili Yake, Peke Yake, pamoja na kutaja jina Lake.
Verse 3
Mwenye kukutukia wewe na kuyatukia uliyokuja nayo ya uongofu na nuru ndiye itakayokatika athari yake na yeye mwenyewe kukatiwa kila kheri.
تقدم القراءة