Tafsiri ya Sura Ad-Dhuhah kwa السواحلية kutoka الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Verse 1
ﮉ
ﮊ
Mwenyezi Mungu Anaapa kwa wakati wa dhuha, na uliokusudiwa ni wakati wa mchana mzima.
Verse 2
ﮋﮌﮍ
ﮎ
Na kwa usiku utuliapo na viumbe na likashadidi giza lake. Mwenyezi Mungu Huapa kwa Atakacho katika viumbe vyake. Ama kiumbe, hafai kuapa kwa asiyekuwa Muumba wake. Kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni ushirikina.
Verse 3
ﮏﮐﮑﮒﮓ
ﮔ
Hakukuwacha Mola wako, ewe Mtume, wala Hakukuchukia kwa kuchelewesha kukuteremshiaWahyi.
Verse 4
ﮕﮖﮗﮘﮙ
ﮚ
Na Nyumba ya Akhera ni bora kwako kuliko nyumba ya ulimwengu.
Verse 5
ﮛﮜﮝﮞ
ﮟ
Na Atakupa Mola wako, ewe Mtume, neema ya kila sampuli uridhike.
Verse 6
ﮠﮡﮢﮣ
ﮤ
Kwani Hakukupata, kabla ya hapo, kuwa ni yatima Akakukusanya na kukutunza.
Verse 7
ﮥﮦﮧ
ﮨ
Na Akakupata hujui Kitabu wala Imani, Akakufundisha yale amabayo ulikuwa huyajui na akakuafikia kufanya amali bora?
Verse 8
ﮩﮪﮫ
ﮬ
Na Akakupata masikini, Akakuletea riziki yako na Akakutajirisha kwa kutosheka na kusubiri?
Verse 9
ﮭﮮﮯﮰ
ﮱ
Basi yatima usimtende ubaya.
Verse 10
ﯓﯔﯕﯖ
ﯗ
Na muombaji usimkaripie, bali mlishe na umtimizie haja yake.
Verse 11
ﯘﯙﯚﯛ
ﯜ
Na ama neema ya Mola wako Aliyokuneemesha nayo izungumze.
تقدم القراءة