ﰉ
surah.translation
.
ﰡ
Mwenyezi Mungu Anaapa kwa usiku unapoifinika ardhi na vilivyoko juu yake kwa giza lake.
Na kwa mchana unapofunuka mwangaza wake kutoka kwenye giza la usiku.
Na kwa kuumba mbea mbili: ya kiume na ya kike,
Kuwa vitendo vyenu vinatofautiana: kuna wenye kufanyia dunia na wenye kufanyia Akhera.
Ama mwenye kutoa kwenye mali yake, akamcha Mwenyezi Mungu katika huko kutoa,
ﯘﯙ
ﰅ
akaamini «Lā Ilāha Illā Allāh» na yanayotakiwa na Imani hiyo na akaamini malipo yanayofungamana nayo,
ﯛﯜ
ﰆ
Tutamuongoza na kumuafikia njia za kheri na wema na kumsahilishia mambo yake.
Na ama mwenye kuyafanyia ubakhili mali yake, asiwe na haja ya malipo ya Mola wake,
ﯣﯤ
ﰈ
akakanusha neno la «Lā Ilāha Illā Allāh» na yanayotakiwa na neno hilo na akakanusha malipo yanayofungamana nalo,
ﭑﭒ
ﰉ
Tutamnyoshea njia za mateso.
Wala hayatamfaa yeye mali yake aliyoyafanyia ubakhili atakapotumbukia Motoni.
Ni juu Yetu, kwa fadhila Zetu na busara Yetu, kueleza njia ya uongofu yenye kufikisha kwa Mwenyezi Mungu na ya upotevu.
Na Sisi Tuna mamlaka ya maisha ya Akhera na maisha ya ulimwenguni.
Ndipo nikawaonya , enyi watu, na kuwatisha moto wenye kuwaka, nao ni moto wa Jahanamu.
Hataingia Moto huo isipokuwa aliyekuwa mbaya sana. Mwenye kumkanusha Nabii Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie,
na akakataa kumwamini na kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake.
ﭱﭲ
ﰐ
Na ataepushwa nao mchaji Mwenyezi Mungu sana.
Ambaye hutoa mali yake kwa kutaka nyongeza za kheri
kutoa Kwake si kwa kulipa zema alizofanyiwa na mtu.
Lakini anatoa kwa kutaka uso wa Mola wake na radhi zake. Basi Mwenyezi Mungu atampa,
ﮆﮇ
ﰔ
huko Peponi, malipo ya kumridhisha.