Tafsiri ya Sura Al-Kafirun kwa السواحلية kutoka الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Verse 1
ﭑﭒﭓ
ﭔ
Sema, ewe Mtume, kuwaambia waliokufuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake: «Enyi wenye kumkanusha Mwenyezi Mungu!
Verse 2
ﭕﭖﭗﭘ
ﭙ
«Mimi siabudu mnavyoviabudu miongoni mwa masanamu na waungu wa urongo.
Verse 3
ﭚﭛﭜﭝﭞ
ﭟ
«Wala nyinyi si wenye kuabudu Mola Mmoja ninayemuabudu Ambaye ndiye Anayestahiki kuabudiwa.
Verse 4
ﭠﭡﭢﭣﭤ
ﭥ
«Wala mimi si mwenye kuabudu mnavyoviabudu miongoni mwa masanamu na waungu wa urongo.
Verse 5
ﭦﭧﭨﭩﭪ
ﭫ
«Wala nyinyi si wenye kuabudu mbeleni ninayemuabudu.» Aya hii imeteremka juu ya watu makhsusi miongoni mwa washirikina ambao Mwenyezi Mungu Alijua kuwa hawataamini kabisa.
Verse 6
ﭬﭭﭮﭯ
ﭰ
«Nyinyi mna dini yenu mnayoiamini na mimi nina Dini yangu ambayo sitaki nyingine.»
تقدم القراءة