Tafsiri ya Sura Abasa kwa السواحلية kutoka الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Verse 1
ﭑﭒ
ﭓ
Yalidhihiri mabadiliko na mkunjiko katika uso wa Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie,
Verse 2
ﭔﭕﭖ
ﭗ
na akapa nyongo kwa sababu ya kwamba Abdallah bin Ummi Maktum alimjilia akitaka aelekezwe. Na alikuwa Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ameshughulika kuwalingania miamba wa Kikureshi katika Uislamu.
Verse 3
ﭘﭙﭚﭛ
ﭜ
Ni kitu gani kinakufanya wewe ujue uhakika wa jambo lake? Kwani huenda ikawa, kwa kuuliza kwake, nafsi yake itatakasika na kusafika.
Verse 4
ﭝﭞﭟﭠ
ﭡ
Au pengine apate mazingatio zaidi na kutishika.
Verse 5
ﭢﭣﭤ
ﭥ
Basi yule alijyejitosheleza na kutouhitajia uongozi wako,
Verse 6
ﭦﭧﭨ
ﭩ
wewe ndiye unayemjali na wapulikiza maneno yake.
Verse 7
ﭪﭫﭬﭭ
ﭮ
Na ni kitu gani kinachokupa jukumu kwako iwapo hakusafika na ukafiri wake?
Verse 8
ﭯﭰﭱﭲ
ﭳ
Ama yule ambaye amekuwa na pupa la kukutana na wewe,
Verse 9
ﭴﭵ
ﭶ
na huku anamuogopa Mwenyezi Mungu asiwe na kasoro katika kupata uongofu,
Verse 10
ﭷﭸﭹ
ﭺ
wewe unampuuza. Ilivyotakikana ufanye si kama ulivyofanya, ewe Mtume.
Verse 11
ﭻﭼﭽ
ﭾ
Hakika Sura hii ni mawaidha kwako na kwa kila anayetaka kuwaidhika.
Verse 12
ﭿﮀﮁ
ﮂ
Basi atakaye atamkumbuka Mwenyezi Mungu na kumtaja na atafuata Wahyi Wake.
Verse 13
ﮃﮄﮅ
ﮆ
Wahyi huu, nao ni Qur’ani, uko katika kurasa zilizotukuzwa,
Verse 14
ﮇﮈ
ﮉ
zenye kuheshimiwa, zenye cheo cha juu,
Verse 15
ﮊﮋ
ﮌ
zilizosafishwa na uchafu, uongezaji na upunguzaji.
Verse 16
ﮍﮎ
ﮏ
Zilizoko mikononi mwa Malaika waandishi, mabalozi kati ya Mwenyezi Mungu na viumbe Wake, wenye maumbile mema, tabia zao ni nzuri na njema na pia matendo yao.
Verse 17
ﮐﮑﮒﮓ
ﮔ
Amelaaniwa mtu kafiri na ataadhibiwa. Ni uovu ulioje wa ukafiri wake kwa Mola wake!
Verse 18
ﮕﮖﮗﮘ
ﮙ
Kwani hajui ni kwa kitu gani Mwenyezi Mungu Alimuumba kwacho mwanzo wake?
Verse 19
ﮚﮛﮜﮝ
ﮞ
Mwenyezi Mungu Alimuumba kwa maji machache, nayo ni manii. Akayakadiria miongo yake.
Verse 20
ﮟﮠﮡ
ﮢ
Kisha Akambainishia njia ya kheri na ya shari.
Verse 21
ﮣﮤﮥ
ﮦ
Kisha humkosesha uhai, na Amemuekea mahali pa kuzikiwa.
Verse 22
ﮧﮨﮩﮪ
ﮫ
Kisha Akitaka Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na sifa mbaya, Atamhuisha na kumfufua baada ya kifo chake, kwa ajili ya kuhesabiwa na kulipwa.
Verse 23
ﮬﮭﮮﮯﮰ
ﮱ
Mambo siyo kama yale anayoyasema kafiri na anayoyafanya. Bado hajatakeleza Aliyomuamrisha kwayo Mwenyezi Mungu katika kuamini na kutenda wema kwa kumtii.
Verse 24
ﯓﯔﯕﯖ
ﯗ
Na azingatie binadamu, vipi Mwenyezi Mungu Amekiumba chakula chake ambacho ndicho kinachoendeleza maisha yake?
Verse 25
ﯘﯙﯚﯛ
ﯜ
Aone kwamba Sisi Tumeyamimina maji ya mvua juu ya ardhi kwa wingi.
Verse 26
ﯝﯞﯟﯠ
ﯡ
Kisha Tumeipasua ardhi kwa Tulivyo vitoa kutoka humo miongoni mwa mimea tofauti.
Verse 27
ﯢﯣﯤ
ﯥ
Tukaotesha humo nafaka
Verse 28
ﯦﯧ
ﯨ
na zabibu, na nyasi za wanyama.Na mizaituni na mitende.
Verse 29
ﯩﯪ
ﯫ
Na mabustani yenye miti mikubwa.
Verse 30
ﯬﯭ
ﯮ
Na matunda
Verse 31
ﯯﯰ
ﯱ
na ndisha.
Verse 32
ﯲﯳﯴ
ﯵ
Mnajistareheshea kwazo, nyinyi na wanyama wenu.
Verse 33
ﯶﯷﯸ
ﯹ
Utakapokuja Ukelele wa Siku ya Kiyama, ambao utayatia uziwi, kwa kitisho chake, masikizi.
Verse 34
ﯺﯻﯼﯽﯾ
ﯿ
Siku mtu atakapomkimbia, kwa kitisho cha Siku Hiyo, nduguye
Verse 35
ﰀﰁ
ﰂ
na babake na mamake na
Verse 36
ﰃﰄ
ﰅ
mkewe na wanawe.
Verse 37
ﰆﰇﰈﰉﰊﰋ
ﰌ
Kila mmoja Siku Hiyo, atakuwa na jambo litakalomzuia asishughulike na mwingine.
Verse 38
ﰍﰎﰏ
ﰐ
Nyuso za wenye neema, Siku Hiyo, zitakuwa ni zenye kung’ara,
Verse 39
ﰑﰒ
ﰓ
zenye furaha na nderemo.
Verse 40
ﰔﰕﰖﰗ
ﰘ
Na nyuso za watu wa Motoni zitakuwa na giza,
Verse 41
ﭑﭒ
ﭓ
nyeusi, zafinikwa na unyonge.
Verse 42
ﭔﭕﭖﭗ
ﭘ
Hao wenye kusifika na sifa hiyo ndiwo wale waliozikufuru neema za Mwenyezi Mungu na wakazikanusha aya zake na wakayakeuka Aliyoyaharamisha kwa kutenda maovu na kukiuka mipaka.
تقدم القراءة