Tafsiri ya Sura Al-zalzalah kwa السواحلية kutoka الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Verse 1
ﮅﮆﮇﮈ
ﮉ
Itakapotikiswa ardhi mtikiso wa nguvu.
Verse 2
ﮊﮋﮌ
ﮍ
Na ikatoa vilivyomo ndani yake: wafu na makandi.
Verse 3
ﮎﮏﮐﮑ
ﮒ
Na akauliza binadamu, kwa babaiko, «Imezukiwa na nini?»
Verse 4
ﮓﮔﮕ
ﮖ
Siku ya Kiyama ardhi itatoa habari ya mambo iliyofanyiwa ya uzuri na ubaya.
Verse 5
ﮗﮘﮙﮚ
ﮛ
kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, Ameiamuru itoe habari ya mambo iliyofanyiwa.
Verse 6
ﮜﮝﮞﮟﮠﮡ
ﮢ
Siku hiyo wataondoka kutoka kwenye kisimamo cha Hesabu wakiwa makundi, ili Mwenyezi Mungu Awaoneshe waliyoyatenda, mazuri na mabaya, na Awalipe kwayo.
Verse 7
ﮣﮤﮥﮦﮧﮨ
ﮩ
Yoyote mwenye kufanya jema wezani wa chungu mdogo atayaona malipo yake Akhera.
Verse 8
ﮪﮫﮬﮭﮮﮯ
ﮰ
Na yoyote mwenye kufanya baya wezani wa chungu mdogo atayaona malipo yake Akhera.
تقدم القراءة