Tafsiri ya Sura Al-zalzalah kwa السواحلية kutoka Ali Muhsin Al - Swahili translation
Verse 1
ﮅﮆﮇﮈ
ﮉ
Al-zalzalah
Itakapo tetemeshwa ardhi kwa mtetemeko wake!
Verse 2
ﮊﮋﮌ
ﮍ
Na itakapo toa ardhi mizigo yake!
Verse 3
ﮎﮏﮐﮑ
ﮒ
Na mtu akasema: Ina nini?
Verse 4
ﮓﮔﮕ
ﮖ
Siku hiyo itahadithia khabari zake.
Verse 5
ﮗﮘﮙﮚ
ﮛ
Kwa sababu Mola wake Mlezi ameifunulia!
Verse 6
ﮜﮝﮞﮟﮠﮡ
ﮢ
Siku hiyo watu watatoka kwa mfarakano wakaonyweshwe vitendo vyao!
Verse 7
ﮣﮤﮥﮦﮧﮨ
ﮩ
Basi anaye tenda chembe ya wema, atauona!
Verse 8
ﮪﮫﮬﮭﮮﮯ
ﮰ
Na anaye tenda chembe ya uovu atauona!
تقدم القراءة