سورة النحل

Ali Muhsin Al - Swahili translation

Tafsiri ya Sura An-Nahl kwa السواحلية kutoka Ali Muhsin Al - Swahili translation

Ali Muhsin Al - Swahili translation


Au hatawashika kwa kitisho na kuwapunguza kidogo kidogo? Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenye huruma, Mwenye kurehemu.

Na wanamfanyia Mwenyezi Mungu ati ana mabinti, Subhanahu, Aliye takasika! Na wao wenyewe, ati ndio wawe na hayo wanayo yatamani!

Na alikwisha wajia Mjumbe wa miongoni mwao wenyewe. Lakini wakamkanusha; basi iliwafika adhabu hali ya kuwa wamedhulumu.
تقدم القراءة