Tafsiri ya Sura Al-Muzzammil kwa السواحلية kutoka Ali Muhsin Al - Swahili translation
Verse 1
ﭑﭒ
ﭓ
Al-Muzzammil
Ewe uliye jifunika!
Verse 2
ﭔﭕﭖﭗ
ﭘ
Kesha usiku kucha, ila kidogo tu!
Verse 3
ﭙﭚﭛﭜﭝ
ﭞ
Nusu yake, au ipunguze kidogo.
Verse 4
ﭟﭠﭡﭢﭣﭤ
ﭥ
Au izidishe - na soma Qur'ani kwa utaratibu na utungo.
Verse 5
ﭦﭧﭨﭩﭪ
ﭫ
Hakika Sisi tutakuteremshia kauli nzito.
Verse 6
Hakika kuamka usiku kunawafikiana zaidi na moyo, na maneno yake yanatua zaidi.
Verse 7
ﭵﭶﭷﭸﭹﭺ
ﭻ
Kwani hakika mchana una shughuli nyingi.
Verse 8
ﭼﭽﭾﭿﮀﮁ
ﮂ
Na lidhukuru jina la Mola wako Mlezi, na ujitolee kwake kwa ukamilifu.
Verse 9
Mola Mlezi wa mashariki na magharibi, hapana mungu isipo kuwa Yeye, basi mfanye kuwa Mtegemewa wako.
Verse 10
Na vumilia hayo wayasemayo, na jitenge nao kwa vizuri.
Verse 11
ﮕﮖﮗﮘﮙﮚ
ﮛ
Na niache Mimi na hao wanao kanusha, walio neemeka; na wape muhula kidogo!
Verse 12
ﮜﮝﮞﮟ
ﮠ
Hakika Sisi tunazo pingu nzito na Moto unao waka kwa ukali kabisa!
Verse 13
ﮡﮢﮣﮤﮥ
ﮦ
Na chakula kinacho kwama kooni, na adhabu inayo umiza.
Verse 14
Siku ambayo ardhi itatikiswa na milima pia, na milima itakuwa kama tifutifu la mchanga!
Verse 15
Hakika Sisi tumemtuma kwenu Mtume aliye shahidi juu yenu, kama tulivyo mtuma Mtume kwa Firauni.
Verse 16
ﯝﯞﯟﯠﯡﯢ
ﯣ
Lakini Firauni alimuasi huyo Mtume, basi tukamshika mshiko wa mateso.
Verse 17
Basi nyinyi mkikufuru, mtawezaje kujikinga na Siku ambayo itawafanya watoto wadogo waote mvi?
Verse 18
Hapo mbingu zitapasuka! Ahadi yake itakuwa imetekelezwa.
Verse 19
Kwa hakika hili ni kumbusho. Mwenye kutaka atashika njia ya kwendea kwa Mola wake Mlezi.
Verse 20
Hakika Mola wako Mlezi anajua ya kuwa hakika wewe unakesha karibu na thuluthi mbili za usiku, na nusu yake, na thuluthi yake. Na baadhi ya watu walio pamoja nawe kadhaalika. Na Mwenyezi Mungu ndiye anaye ukadiria usiku na mchana. Anajua kuwa hamwezi kuweka hisabu, basi amekusameheni. Basi someni kilicho chepesi katika Qur'ani. Anajua ya kuwa baadhi yenu watakuwa wagonjwa, na wengine wanasafiri katika ardhi wakitafuta fadhila ya Mwenyezi Mungu, na wengine wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo someni kilicho chepesi humo, na mshike Sala, na toeni Zaka, na mkopesheni Mwenyezi Mungu mkopo mwema. Na kheri yoyote mnayo itanguliza kwa ajili ya nafsi zenu mtaikuta kwa Mwenyezi Mungu, imekuwa bora zaidi, na ina thawabu kubwa sana. Na mtakeni msamaha Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.
تقدم القراءة