Tafsiri ya Sura Nouh kwa السواحلية kutoka Ali Muhsin Al - Swahili translation
Verse 1
Nouh
Hakika Sisi tulimtuma Nuh'u kwa watu wake: Uwaonye kaumu yako kabla ya kuwafikia adhabu chungu.
Verse 2
ﮇﮈﮉﮊﮋﮌ
ﮍ
Akasema: Enyi watu wangu! Kwa hakika mimi ni mwonyaji wa dhaahiri kwenu,
Verse 3
ﮎﮏﮐﮑﮒ
ﮓ
Ya kwamba mumuabudu Mwenyezi Mungu, na mumche Yeye, na mumt'ii.
Verse 4
Atakughufirieni madhambi yenu, na atakuakhirisheni mpaka muda ulio wekwa. Hakika muda wa Mwenyezi Mungu utapo fika haucheleweshwi. Laiti mngejua!
Verse 5
Akasema: Ee Mola wangu Mlezi! Hakika mimi nimewaita watu wangu usiku na mchana,
Verse 6
ﮱﯓﯔﯕﯖ
ﯗ
Lakini wito wangu haukuwazidisha ila kukimbia.
Verse 7
Na hakika mimi kila nilipo waita ili upate kuwaghufiria, walijiziba masikio yao kwa vidole vyao, na wakajigubika nguo zao, na wakakamia, na wakatakabari vikubwa mno!
Verse 8
ﯧﯨﯩﯪ
ﯫ
Tena niliwaita kwa uwazi,
Verse 9
Kisha nikawatangazia kwa kelele, tena nikasema nao kwa siri.
Verse 10
ﯴﯵﯶﯷﯸﯹ
ﯺ
Nikasema: Ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi; hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe.
Verse 11
ﭑﭒﭓﭔ
ﭕ
Atakuleteeni mvua inyeshe mfululizo.
Verse 12
Na atakupeni mali na wana, na atakupeni mabustani na atakufanyieni mito.
Verse 13
ﭠﭡﭢﭣﭤﭥ
ﭦ
Mna nini hamweki heshima ya Mwenyezi Mungu?
Verse 14
ﭧﭨﭩ
ﭪ
Na hali Yeye kakuumbeni daraja baada ya daraja?
Verse 15
Kwani hamwoni jinsi Mwenyezi Mungu alivyo ziumba mbingu saba kwa matabaka?
Verse 16
Na akaufanya mwezi ndani yake uwe nuru, na akalifanya jua kuwa taa?
Verse 17
ﭼﭽﭾﭿﮀ
ﮁ
Na Mwenyezi Mungu amekuotesheni katika ardhi kama mimea.
Verse 18
ﮂﮃﮄﮅﮆ
ﮇ
Kisha atakurudsheni humo na atakutoeni tena.
Verse 19
ﮈﮉﮊﮋﮌ
ﮍ
Na Mwenyezi Mungu amekukunjulieni ardhi kama busati.
Verse 20
ﮎﮏﮐﮑ
ﮒ
Ili mtembee humo katika njia zilizo pana.
Verse 21
Nuh'u akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika hao wameniasi, na wamemfuata yule ambaye mali yake na wanawe hawakumzidishia ila khasara.
Verse 22
ﮡﮢﮣ
ﮤ
Na wakapanga vitimbi vikubwa.
Verse 23
Na wakasema: Msiwaache miungu yenu, wala msimwache Wadda wala Suwaa' wala Yaghutha, wala Yau'qa, wala Nasra.
Verse 24
Na hao walikwisha wapoteza wengi, wala usiwazidishie walio dhulumu ila kupotea.
Verse 25
Basi kwa ajili ya makosa yao waligharikishwa wakaingizwa Motoni, wala hawakuwapata wa kuwanusuru badala ya Mwenyezi Mungu.
Verse 26
Na Nuh'u akasema: Mola wangu Mlezi! Usimwache juu ya ardhi mkaazi wake yeyote katika makafiri!
Verse 27
Hakika ukiwaacha watawapoteza waja wako, wala wao hawatazaa ila waovu makafiri.
Verse 28
Mola wangu Mlezi! Nighufirie mimi na wazazi wangu, na kila aliye ingia nyumbani mwangu kuwa ni mwenye kuamini, na Waumini wote wanaume, na Waumini wanawake. Na wala usiwazidishie walio dhulumu ila kupotea.
تقدم القراءة