Tafsiri ya Sura Marya kwa السواحلية kutoka Ali Muhsin Al - Swahili translation
Verse 1
ﭑ
ﭒ
Marya
Kaf Ha Ya A'yn S'ad
Verse 2
ﭓﭔﭕﭖﭗ
ﭘ
Huu ni Ukumbusho wa rehema ya Mola wako Mlezi kwa mja wake, Zakariya.
Verse 3
ﭙﭚﭛﭜﭝ
ﭞ
Alipo mwita Mola wake Mlezi kwa siri.
Verse 4
Akasema: Mola wangu Mlezi! Mafupa yangu yamedhoofika, na kichwa kinameremeta kwa mvi; wala, Mola wangu Mlezi, sikuwa mwenye bahati mbaya kwa kukuomba Wewe.
Verse 5
Na hakika mimi nawakhofia jamaa zangu baada yangu. Na mke wangu ni tasa. Basi nipe mrithi kutoka kwako.
Verse 6
Atakaye nirithi mimi na awarithi ukoo wa Yaaqub. Ewe Mola wangu Mlezi! Na umjaalie awe mwenye kuridhisha.
Verse 7
(Akaambiwa): Ewe Zakariya! Hakika Sisi tunakubashiria mwana; jina lake ni Yahya. Hatujapata kumpa jina hilo yeyote kabla yake.
Verse 8
Akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Vipi nitakuwa na mwana na hali mke wangu ni tasa, na mimi nimesha fikia ukongwe katika uzee?
Verse 9
Akasema: Ndio hivyo hivyo amesema Mola wako Mlezi: Haya ni mepesi kwangu. Na hakika Mimi nilikwisha kuumba wewe zamani na hali hukuwa kitu.
Verse 10
Akasema: Mola wangu Mlezi nijaalie Ishara. Akasema Ishara yako ni kuwa hutasema na watu kwa masiku matatu, na hali ni mzima.
Verse 11
Basi akawatokea watu wake kutoka mihirabuni. Akawaashiria: Msabihini Mwenyezi Mungu asubuhi na jioni.
Verse 12
Ewe Yahya! Kishike Kitabu kwa nguvu! Nasi tulimpa hikima angali mtoto.
Verse 13
Na tukampa huruma itokayo kwetu, na utakaso, na akawa mchamungu.
Verse 14
ﭢﭣﭤﭥﭦﭧ
ﭨ
Na akawa mwema kwa wazazi wake, wala hakuwa jabari mua'si.
Verse 15
Na amani iwe juu yake siku ya kuzaliwa, na siku ya kufa, na siku ya kufufuliwa.
Verse 16
Na mtaje Maryamu katika Kitabu, pale alipo jitenga na jamaa zake mahali upande wa mashariki;
Verse 17
Na akaweka pazia kujikinga nao. Tukampelekea Roho wetu, akajifananisha kwake sawa na mtu.
Verse 18
(Maryamu) akasema: Hakika mimi najikinga kwa Mwingi wa Rehema aniepushe nawe, ukiwa ni mchamngu.
Verse 19
(Malaika) akasema: Hakika mimi ni mwenye kutumwa na Mola wako Mlezi ili nikubashirie tunu ya mwana aliye takasika.
Verse 20
Akasema: Nitampataje mwana hali mwanaadamu yeyote hajanigusa, wala mimi si kahaba?
Verse 21
(Malaika) akasema: Ndio hivyo hivyo! Mola wako Mlezi amesema: Haya ni mepesi kwangu! Na ili tumfanye kuwa ni Ishara kwa watu, na Rehema itokayo kwetu, na hilo ni jambo lilio kwisha hukumiwa.
Verse 22
ﯜﯝﯞﯟﯠﯡ
ﯢ
Basi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali.
Verse 23
Kisha uchungu ukampeleka kwenye shina la mtende; akasema: Laiti ningeli kufa kabla ya haya, na nikawa niliye sahaulika kabisa!
Verse 24
Pakatangazwa kutoka chini yake: Usihuzunike! Hakika Mola wako Mlezi amejaalia chini yako kijito kidogo cha maji!
Verse 25
Na litikise kwako hilo shina la mtende, utakuangushia tende nzuri zilizo mbivu.
Verse 26
Basi kula, na kunywa, na litue jicho lako. Na pindi ukimwona mtu yeyote basi sema: Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kufunga; kwa hivyo leo sitasema na mtu.
Verse 27
Akenda naye (mwanawe) kwa jamaa zake amembeba. Wakasema: Ewe Maryamu! Hakika umeleta kitu cha ajabu!
Verse 28
Ewe dada yake Harun! Baba yako hakuwa mtu muovu, wala mama yako hakuwa kahaba.
Verse 29
Akawaashiria (mtoto). Wakasema: Vipi tumsemeze aliye bado mdogo yumo katika mlezi?
Verse 30
(Mtoto) akasema: Hakika mimi ni mtumwa wa Mwenyezi Mungu. Amenipa Kitabu, na amenifanya Nabii.
Verse 31
Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Sala na Zaka maadamu ni hai,
Verse 32
ﮞﮟﮠﮡﮢﮣ
ﮤ
Na nimtendee wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, mwovu.
Verse 33
Na amani iko juu yangu siku niliyo zaliwa, na siku nitakayo kufa, na siku nitakayo fufuliwa kuwa hai.
Verse 34
Huyo ndiye Isa mwana wa Maryamu. Ndiyo kauli ya haki ambayo wanaifanyia shaka.
Verse 35
Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwa na mwana, Subhanahu, Yeye ametakasika! Anapo lihukumia jambo basi huliambia tu: Kuwa! Likawa.
Verse 36
Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu Mlezi, na Mola wenu Mlezi. Basi muabuduni Yeye. Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka.
Verse 37
Lakini makundi yakakhitalifiana wao kwa wao. Basi ole wao hao walio kufuru kwa kuhudhuria Siku iliyo kuu!
Verse 38
Watasikia na wataona vizuri vilioje Siku watakayo tufikia! Lakini madhaalimu sasa wamo katika upotofu ulio dhaahiri.
Verse 39
Na waonye siku ya majuto itapo katwa amri. Nao wamo katika ghafla, wala hawaamini.
Verse 40
Hakika Sisi tutairithi ardhi na walio juu yake. Na kwetu watarejeshwa.
Verse 41
Na mtaje katika Kitabu Ibrahim. Hakika yeye alikuwa mkweli, Nabii.
Verse 42
Alipo mwambia baba yake: Ewe baba yangu! Kwa nini unaabudu visivyo sikia, na visivyo ona, na visivyo kufaa chochote?
Verse 43
Ewe baba yangu! Kwa yakini imenifikia ilimu isiyo kufikia wewe. Basi nifuate mimi, nami nitakuongoza Njia Iliyo Sawa.
Verse 44
Ewe baba yangu! Usimuabudu Shet'ani. Hakika Shet'ani ni mwenye kumuasi Mwingi wa Rehema.
Verse 45
Ewe baba yangu! Hakika mimi naogopa isikupate adhabu inayo toka kwa Mwingi wa Rehema ukaja kuwa mwenziwe Shet'ani.
Verse 46
(Baba) akasema: Unaichukia miungu yangu, ewe Ibrahim? Kama huachi, basi lazima nitakupiga mawe. Na niondokelee mbali kwa muda!
Verse 47
(Ibrahim) akasema: Salamun a'laika! Amani iwe juu yako! Mimi nitakuombea msamaha kwa Mola wangu Mlezi. Hakika Yeye ananihurumia sana.
Verse 48
Nami najitenga nanyi na hayo mnayo yaabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Na ninamwomba Mola wangu Mlezi; asaa nisiwe mwenye kukosa bahati kwa kumwomba Mola wangu Mlezi.
Verse 49
Basi alipo jitenga nao na yale waliyo kuwa wakiyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, tulimpa Is-haq na Yaaqub, na kila mmoja tukamfanya Nabii.
Verse 50
Na tukawapa rehema zetu na tukawajaalia kupewa sifa za kweli tukufu.
Verse 51
Na mtaje Musa katika Kitabu. Hakika yeye alikuwa ni mwenye kuchaguliwa, na alikuwa Mtume, Nabii.
Verse 52
Na tulimwita upande wa kulia wa mlima na tukamsogeza kunong'ona naye.
Verse 53
Nasi kwa rehema zetu tukampa nduguye, Harun, awe Nabii.
Verse 54
Na mtaje katika Kitabu Ismail. Bila ya shaka yeye alikuwa ni mkweli wa ahadi, na alikuwa Mtume, Nabii.
Verse 55
Na alikuwa akiwaamrisha watu wake Sala na Zaka, na alikuwa mbele ya Mola wake Mlezi mwenye kuridhiwa.
Verse 56
Na mtaje katika Kitabu Idris. Hakika yeye alikuwa ni mkweli Nabii.
Verse 57
ﮂﮃﮄ
ﮅ
Na tulimuinua daraja ya juu.
Verse 58
Hao ndio alio waneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii katika uzao wa Adam, na katika uzao wa wale tulio wapandisha pamoja na Nuhu, na katika uzao wa Ibrahim na Israil, na katika wale tulio waongoa na tukawateuwa. Wanapo somewa Aya za Mwingi wa Rehema huanguka kusujudu na kulia.
Verse 59
Lakini wakaja baada yao walio wabaya, wakaacha Sala, na wakafuata matamanio. Basi watakuja kuta malipo ya ubaya.
Verse 60
Isipo kuwa walio tubu, wakaamini, na wakatenda mema. Hao, basi, wataingia Peponi wala hawatadhulumiwa chochote.
Verse 61
Bustani za milele alizo waahidi Rahmani waja wake katika siri. Hakika ahadi yake hapana shaka itafika.
Verse 62
Humo hawatasikia upuuzi, ila Salama tu. Na watapata humo riziki zao asubuhi na jioni.
Verse 63
Hiyo ndiyo Pepo tutayo warithisha katika waja wetu walio kuwa wachamngu.
Verse 64
(Nao watasema:) Wala hatuteremki ila kwa amri ya Mola wako Mlezi. Ni yake Yeye yaliyoko mbele yetu na yaliyoko nyuma yetu, na yaliyomo katikati ya hayo. Na Mola wako Mlezi si mwenye kusahau.
Verse 65
Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake. Basi muabudu Yeye tu, na udumu katika ibada yake. Je, mnamjua mwenye jina kama lake?
Verse 66
Na mwanaadamu husema: Hivyo, nitakapo kufa, ni kweli nitafufuliwa niwe hai tena?
Verse 67
Je! Hakumbuki mwanaadamu ya kwamba tulimuumba kabla, na hali hakuwa chochote?
Verse 68
Basi naapa kwa Mola wako Mlezi! Kwa yakini tutawakusanya wao pamoja na mashet'ani; kisha tutawahudhurisha kuizunguka Jahannamu, nao wamepiga magoti!
Verse 69
Kisha kwa yakini tutawatoa katika kila kundi wale miongoni mwao walio zidi kumuasi Arrahmani, Mwingi wa Rahema..
Verse 70
Tena hakika Sisi tunawajua vyema zaidi wanao stahiki kuunguzwa humo.
Verse 71
Wala hapana yeyote katika nyinyi ila ni mwenye kuifikia. Hiyo ni hukumu ya Mola wako Mlezi ambayo lazima itimizwe.
Verse 72
Kisha tutawaokoa wale walio mchamngu; na tutawaacha madhaalimu humo wamepiga magoti.
Verse 73
Na wanapo somewa Aya zetu zilizo wazi, walio kufuru huwaambia walio amini: Lipi katika makundi mawili lenye cheo kizuri na lilio bora barazani?
Verse 74
Na kaumu ngapi tuliziangamiza zilizo kuwa na mapambo mazuri zaidi na wazuri zaidi kwa kuwatazama!
Verse 75
Sema: Walio katika upotofu basi Arrahmani Mwingi wa Rahema atawapururia muda mpaka wayaone waliyo onywa - ama ni adhabu au ni Saa. Hapo ndipo watapo jua ni nani mwenye makao mabaya na mwenye askari dhaifu.
Verse 76
Na Mwenyezi Mungu huwazidishia uwongofu wenye kushika uwongofu. Na mema yenye kudumu ni bora katika malipo mbele ya Mola wako Mlezi na yana mwisho mwema.
Verse 77
Je, umemwona aliye zikanya Ishara zetu na akasema: Kwa hakika mimi nitapewa mali na wana!
Verse 78
Kwani yeye amepata khabari za ghaibu, au amechukua ahadi kwa Arrahmani Mwingi wa Rehema?
Verse 79
Hasha! Tutaandika anayo yasema, tutamkunjulia muda wa adhabu.
Verse 80
ﭭﭮﭯﭰﭱ
ﭲ
Na tutamrithi hayo anayo yasema, na atatufikia mtupu peke yake!
Verse 81
Na wamechukua miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu ili ati iwape nguvu.
Verse 82
Sivyo kabisa! Wataikataa hiyo ibada yao, na watakuwa ndio dhidi yao.
Verse 83
Kwani huoni ya kwamba tumewatuma mashet'ani kwa makafiri wawachochee kwa uchochezi?
Verse 84
Basi usiwafanyie haraka. Sisi tunawahisabia idadi ya siku zao.
Verse 85
ﮗﮘﮙﮚﮛﮜ
ﮝ
Siku tutayo wakusanya wachamngu kuwapeleka kwa Arrahmani Mwingi wa Rehema kuwa ni wageni wake.
Verse 86
ﮞﮟﮠﮡﮢ
ﮣ
Na tukawachunga wakhalifu kuwapeleka Jahannamu hali ya kuwa wana kiu.
Verse 87
Hawatakuwa na mamlaka ya uombezi ila wale walio chukua ahadi kwa Arrahmani Mwingi wa Rehema..
Verse 88
ﮮﮯﮰﮱ
ﯓ
Na wao ati husema kuwa Arrahmani Mwingi wa Rehema ana mwana!
Verse 89
ﯔﯕﯖﯗ
ﯘ
Hakika mmeleta jambo la kuchusha mno!
Verse 90
Zinakaribia mbingu kutatuka kwa hilo, na ardhi kupasuka, na milima kuanguka vipande vipande.
Verse 91
ﯣﯤﯥﯦ
ﯧ
Kwa kudai kwao kuwa Arrahmani Mwingi wa Rehema ana mwana.
Verse 92
ﯨﯩﯪﯫﯬﯭ
ﯮ
Wala hahitajii Arrahmani Mwingi wa Rehema kuwa na mwana.
Verse 93
Hapana yeyote aliomo mbinguni na ardhini ila atafika kwa Arrahmani Mwingi wa Rehema kuwa ni mtumwa wake.
Verse 94
ﯺﯻﯼﯽ
ﯾ
Yeye hakika amewadhibiti na amewahisabu sawa sawa.
Verse 95
ﯿﰀﰁﰂﰃ
ﰄ
Na kila mmoja katika wao atamfikia Siku ya Kiyama peke yake.
Verse 96
Hakika walio amini na wakatenda mema Arrahmani Mwingi wa Rehema atawajaalia mapenzi.
Verse 97
Na hakika tumeifanya nyepesi (Qur'ani) kwa ulimi wako, ili uwabashirie kwayo wachamngu, na uwaonye kwayo watu wabishi.
Verse 98
Na kaumu ngapi tumezihiliki kabla yao. Je! Unawaona hata mmoja katika wao au unasikia hata mchakato wao?
تقدم القراءة