Tafsiri ya Sura At-Takasur kwa السواحلية kutoka Ali Muhsin Al - Swahili translation
Verse 1
ﮣﮤ
ﮥ
At-Takasur
Kumekushughulisheni kutafuta wingi,
Verse 2
ﮦﮧﮨ
ﮩ
Mpaka mje makaburini!
Verse 3
ﮪﮫﮬ
ﮭ
Sivyo hivyo! Mtakuja jua!
Verse 4
ﮮﮯﮰﮱ
ﯓ
Tena sivyo hivyo! Mtakuja jua!
Verse 5
ﯔﯕﯖﯗﯘ
ﯙ
Sivyo hivyo! Lau mngeli jua kwa ujuzi wa yakini,
Verse 6
ﯚﯛ
ﯜ
Basi bila ya shaka mtaiona Jahannamu!
Verse 7
ﯝﯞﯟﯠ
ﯡ
Tena, bila ya shaka, mtaiona kwa jicho la yakini.
Verse 8
ﯢﯣﯤﯥﯦ
ﯧ
Tena bila ya shaka mtaulizwa siku hiyo juu ya neema.
تقدم القراءة