Tafsiri ya Sura Ad-Dhuhah kwa السواحلية kutoka Ali Muhsin Al - Swahili translation
Verse 1
ﮉ
ﮊ
Ad-Dhuhah
Naapa kwa mchana!
Verse 2
ﮋﮌﮍ
ﮎ
Na kwa usiku unapo tanda!
Verse 3
ﮏﮐﮑﮒﮓ
ﮔ
Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe.
Verse 4
ﮕﮖﮗﮘﮙ
ﮚ
Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia.
Verse 5
ﮛﮜﮝﮞ
ﮟ
Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike.
Verse 6
ﮠﮡﮢﮣ
ﮤ
Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi?
Verse 7
ﮥﮦﮧ
ﮨ
Na akakukuta umepotea akakuongoa?
Verse 8
ﮩﮪﮫ
ﮬ
Akakukuta mhitaji akakutosheleza?
Verse 9
ﮭﮮﮯﮰ
ﮱ
Basi yatima usimwonee!
Verse 10
ﯓﯔﯕﯖ
ﯗ
Na anaye omba au kuuliza usimkaripie!
Verse 11
ﯘﯙﯚﯛ
ﯜ
Na neema za Mola wako Mlezi zisimlie.
تقدم القراءة