Tafsiri ya Sura Al-Mursalat kwa السواحلية kutoka الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Verse 1
ﮑﮒ
ﮓ
Anaapa Mwenyezi Mungu kwa upepo unapovuma kwa mfululizo, huu baada ya huu.
Verse 2
ﮔﮕ
ﮖ
Na kwa upepo wenye kuvuma kwa ukali wenye kuangamiza.
Verse 3
ﮗﮘ
ﮙ
Na kwa Malaika waliopewa jukumu la mawingu, wakawa wayapeleka pale anapotaka Mwenyezi Mungu.
Verse 4
ﮚﮛ
ﮜ
Na kwa Malaika wanaoshuka, kutoka kwa Mwenyezi Mungu,
Verse 5
ﮝﮞ
ﮟ
na amri zinazopambanua baina ya haki na batili na halali na haramu.
Verse 6
ﮠﮡﮢ
ﮣ
Na kwa Malaika wanaoupokea wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kuuteremsha kwa Manabii Wake, unaowapa viumbe wake udhuru kutoka kwa Mwenyezi Mungu na pia onyo kutoka Kwake, ili watu wasiwe na hoja.
Verse 7
ﮤﮥﮦ
ﮧ
Hakika jambo la Kiyama mnaloahidiwa pamoja na lile la kuhesabiwa na kulipwa ni lenye kuwa hapana shaka.
Verse 8
ﮨﮩﮪ
ﮫ
Basi nyota zitakapofutwa na mwangaza wake ukaondoka,
Verse 9
ﮬﮭﮮ
ﮯ
na mbingu zitakapopasuka,
Verse 10
ﮰﮱﯓ
ﯔ
na majabali yatakapopeperuka na kukueanea huku na kule na yakawa ni mapepe yanayorushwa na upepo,
Verse 11
ﯕﯖﯗ
ﯘ
Na Mitume watapowekewa wakati na muda wa baina yao na ummah wao na kusemwe,
Verse 12
ﯙﯚﯛ
ﯜ
«Ni Siku kubwa gani Mitume wameahirishiwa?»
Verse 13
ﯝﯞ
ﯟ
Wameahirishiwa Siku ya hukumu na uamuzi baina ya viumbe.
Verse 14
ﯠﯡﯢﯣﯤ
ﯥ
Na nilipi lililokujulisha wewe, ewe binadamu, ni siku gani hiyo ya kutolewa uamuzi na ni zipi shida zake na vituko vyake?
Verse 15
ﯦﯧﯨ
ﯩ
Maangamivu makubwa Siku hiyo ni ya wale waliyoikanusha Siku hii iliyoahidiwa.
Verse 16
ﯪﯫﯬ
ﯭ
Kwani hatukuawaangamiza walitangulia kati ya umma waliopita kwa kuwakanusha kwao Mitume, kama vile watu wa Nūḥ, ‘Ād na Thamūd?
Verse 17
ﯮﯯﯰ
ﯱ
Kisha tutawakutanisha na wao wale waliokuja nyuma kati ya wale waliokuwa ni kama wao katika ukanushaji na uasi.
Verse 18
ﯲﯳﯴ
ﯵ
Mfano wa uangamizaji huo mkali ndivyo tutakavyowafanya wahalifu kati ya makafiri wa Makkah, kwa kumkanusha kwao Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie.
Verse 19
ﯶﯷﯸ
ﯹ
Maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama kwa kila mwenye kuukanusha upweke wa Mwenyezi Mungu, unabii, kufufuliwa na kuhesabiwa.
Verse 20
ﭑﭒﭓﭔﭕ
ﭖ
Je kwani sisi hatukuwaumba nyinyi, enyi mkusanyiko wa makafiri, kutokana na maji dhaifu yaliyo matwevu nayo ni tone la manii,
Verse 21
ﭗﭘﭙﭚ
ﭛ
tukayaweka maji haya kwenye mahali palipohifadhika, napo ni kizazi cha mwanamke,
Verse 22
ﭜﭝﭞ
ﭟ
mpaka kipindi maalumu kinachojulikana na Mwenyezi Mungu Aliyetukuka?
Verse 23
ﭠﭡﭢ
ﭣ
Tukaweza kumuumba, kumtia sura na kumtoa. Basi bora wa wenye kuweza ni s isi.
Verse 24
ﭤﭥﭦ
ﭧ
Maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama kwa wenye kukanusha uweza wetu.
Verse 25
ﭨﭩﭪﭫ
ﭬ
Je kwani hatukuifanya hii ardhi mnayoishi juu yake
Verse 26
ﭭﭮ
ﭯ
ikusanye juu ya mgongo wake walio hai wasiohesabika, na ndani ya matumbo yake wafu wasiodhibitika, na
Verse 27
tukajaalia iwe na majabali yaliyojikita yaliyo marefu ili isitikisike na nyinyi, na tukawanywesha maji tamu yaliyo mazuri?
Verse 28
ﭸﭹﭺ
ﭻ
Maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama kwa waliozikanusha neema hizi.
Verse 29
ﭼﭽﭾﭿﮀﮁ
ﮂ
Wataambiwa makafiri Siku ya Kiyama, «Endeni kwenye adhabu ya moto wa Jahanamu mliokuwa mkiukanusha duniani.
Verse 30
ﮃﮄﮅﮆﮇﮈ
ﮉ
Endeni mjifinike kwenye kivuli cha moshi wa moto wa Jahanamu ambacho hapo panachembuka vipande vitatu.
Verse 31
ﮊﮋﮌﮍﮎﮏ
ﮐ
Kivuli hiko hakimfanyi mtu ahifadhike na joto la Siku hiyo wala hakizuii muwako wa Moto chochote.
Verse 32
ﮑﮒﮓﮔ
ﮕ
Hakika moto wa Jahanamu unarusha macheche makubwa ya moto, kila cheche moja katika hayo ni kama jengo lililoimarishwa katika ukubwa na urefu wa kuenda juu.
Verse 33
ﮖﮗﮘ
ﮙ
Kama kwamba hizo cheche za moto wa Jahanamu zinazopaa juu ni ngamia weusi ambao rangi yao imeingia kwenye umanjano.»
Verse 34
ﮚﮛﮜ
ﮝ
Maangamivu na adhabu kali kwa wenye kukanusha mateso yaliyoahidiwa na Mwenyezi Mungu.
Verse 35
ﮞﮟﮠﮡ
ﮢ
Hii ndiyo Siku ya Kiyama ambayo wakanushaji hawatatamka maneno ya kuwanufaisha
Verse 36
ﮣﮤﮥﮦ
ﮧ
wala hawatapewa idhini ya kusema wakatoa nyudhuru, kwa kuwa hawatakuwa na udhuru wowote.
Verse 37
ﮨﮩﮪ
ﮫ
Maangamivu na adhabu kali kwa wenye kuikanusha siku hii na yaliyomo ndani yake.
Verse 38
ﮬﮭﮮﮯﮰﮱ
ﯓ
Hii ni Siku ambayo Mwenyezi Mungu Atatoa uamuzi baina ya viumbe, na ukweli na ubatilifu utapambanuka. Tutawakusanya nyinyi Siku hiyo, enyi makafiri wa ummah huu, pamoja na makafiri wa mwanzo miongoni mwa ummah waliopita.
Verse 39
ﯔﯕﯖﯗﯘ
ﯙ
Basi mkiwa na hila za kujitoa na adhabu, tumieni hila zenu na mziokoe nafsi zenu na msukosuko wa Mwenyezi Mungu na mateso Yake.
Verse 40
ﯚﯛﯜ
ﯝ
Maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama kwa wenye kuikanusha Siku ya Kiyama.
Verse 41
ﯞﯟﯠﯡﯢ
ﯣ
Hakika ya wale waliomuogopa Mola wao duniani na wakaiogopa adhabu Yake kwa kufuata amri Zake na kujiepusha na makatazo Yake. Wao Siku ya Kiyama watakuwa kwenye vivuli vya miti vilivyonyoka, na chemchemi za maji zinazotembea,
Verse 42
ﯤﯥﯦ
ﯧ
na matunda mengi yanayopendwa na nafsi zao ambayo wao wanastarehe nayo. Hapo waambiwe,
Verse 43
ﯨﯩﯪﯫﯬﯭ
ﯮ
«Kuleni chakula chenye ladha na mnyweni kinywaji chenye kufurahisha kwa sababu ya matendo mema mliyoyatanguliza duniani.»
Verse 44
ﯯﯰﯱﯲ
ﯳ
Sisi, kwa mfano wa malipo hayo makubwa, tutawalipa watu wema katika matendo yao na utiifu wao kwetu.
Verse 45
ﯴﯵﯶ
ﯷ
Maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama kwa wenye kuikanusha Siku ya Malipo na Hesabu, na kuzikanusha sterehe na mateso yaliyomo Siku hiyo.
Verse 46
ﯸﯹﯺﯻﯼ
ﯽ
Kisha Mwenyezi Mungu Akawaonya makafiri kwa kusema, «Kuleni aina ya vyakula vya ladha duniani na stareheni kwa matamanio yake yenye kumalizika kwa muda mchache, hakika nyinyi ni wahalifu kwa kumshirikisha kwenu Mwenyezi Mungu.»
Verse 47
ﯾﯿﰀ
ﰁ
Maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama kwa wenye kuikanusha Siku ya kuhesabiwa na kulipwa.
Verse 48
ﰂﰃﰄﰅﰆﰇ
ﰈ
Na wanapoambiwa hawa washirikina, «Mswalieni Mwenyezi Mungu na mnyenyekeeni,» hawanyenyekei wala hawaswali, bali wanaendelea kuonyesha kiburi chao.
Verse 49
ﰉﰊﰋ
ﰌ
Maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama kwa wenye kuzikanusha aya za Mwenyezi Mungu.
Verse 50
ﰍﰎﰏﰐ
ﰑ
Iwapo wao hawataiamini hii Qur’ani, basi wataamini kitabu gani na maneno gani baada yake? Na Qur’ani yenyewe ni Kitabu kilichobainisha kila kitu, kilicho wazi katika hekima zake, hukumu zake na habari zake, chenye kushinda katika matamko yake na maana yake.
تقدم القراءة