ترجمة سورة الطارق

الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
ترجمة معاني سورة الطارق باللغة السواحلية من كتاب الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس .

Mwenyezi Mungu Anaapa kwa mbingu na nyota yenye kuchomoza usiku.
Na ni lipi lilokujulisha ni ukubwa gani wa nyota hiyo?
Hiyo ni nyota ing’arao na kuzagaa.
Hakuna nafsi yoyote isipokuwa amewakilishwa kwayo Malaika mwenye kuchunguza na kusjili amali zake ili ihesabiwe Siku ya Kiyama.
Basi aangalie binadamu mwenye kukanusha kufufuliwa ameumbwa kwa kitu gani? Ili ajue kuwa kurudisha umbo lake mara ya pili si vigumu kama kuumbwa mara ya kwanza.
Aliumbwa kwa manii yenye kupenyeza ndani ya uzao kwa haraka.
Yatokayo kwenye mgongo wa mwnamume na kifua cha mwanamke.
Hakika yule Aliyemuumba binadamu kwa maji haya ni muweza wa kumrudisha kwenye uhai baada ya kufa.
Siku zitakapofunuliwa wazi siri ziliofichwa na nafsi na kupambanuliwa njema na mbovu.
Binadamu hatakuwa na nguvu ya kuitetea nafsi yake wala hatakuwa na mtetezi wa kumwepushia adhabu ya Mwenyezi Mungu.
Na Anaapa kwa mbingu yenye mvua ya kukaririka.
Na ardhi yenye pasuko za kufanya mimea ichipuke.
Hakika Qur’ani ni neno lenye kupambanua baina ya haki na batili.
Na si upuuzi. Haifai kiumbe kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Akifanya hivyo atakuwa amemshirikisha Mwenyezi Mungu.
Hakika wenye kumkanusha Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na Qur’ani wanafanya vitimbi na mipango ili kuipinga haki na kuitilia nguvu batili.
Na Mimi nafanya vitimbi kuidhihirisha haki ingawa makafiri wanatukia.Usiwe na haraka nao, ewe Mtume, kutaka wateremshiwe adhabu.
Wape muhula uwangojee muda mchache wala usiwafanyie haraka, utaona adhabu itakayowafikia, mateso na maangamivu.
Icon