ترجمة سورة المسد

الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
ترجمة معاني سورة المسد باللغة السواحلية من كتاب الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس .

Imehasirika mikono miwili ya Abu Lahab, na yeye mwenyewe ameangamia, kwa kumuudhi Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. Hasara ya Abu Lahab ilithubutu.
Hayakumfalia kitu mali yake na watoto wake. Kwani hivyo havitamkinga na adhabu ya Mwenyezi Mungu pindi ikimshukia.
Ataingia kwenye Moto wenye kuroroma,
yeye na mke wake ambaye alikuwa akibeba miba na kuiweka kwenye njia anayopita Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ili kumuudhi.
Kwenye shingo yake patakuwa na kamba imara ya lifu gumu lilio kavu; atabebewa nayo kwenye Moto wa Jahanamu, kisha atarushwa nayo mpaka chini.
Icon